JINSI YA KUANDIKA BARUA YA KIKAZI
Utajifunza
- Lengo la kuandika
barua ya kikazi
- Ukubwa
wa barua yako?
- Jinsi ya
kulinganisha barua yako iendane na kazi unayoomba
- Nini kinatakiwa
kwenye barua yako
- Kipi
kisichotakiwa kwenye barua yako
- Aina tofauti ya
barua za kikazi
Pia Makala hii
itakuonyesha:
- Jinsi ya kuandika barua bora yenye asilimia 9 kati ya
10.
- Utaona mfano wa barua ambao utapelekea kuitwa kwenye
Usahili/interviews (na kwanini).
- Utajifunza mbinu mbalimbali za kuandika barua
itakayopelekea upate kazi kiurahisi
- Utajifunza jinsi ya kuanza naa kumaliza barua yako na
jinsi ya kuiwasilisha.
Barua
ya kikazi ni barua inayoandikwa kwa ukurasa mmoja ambayo inaambatanishwa wakati
wa maombi ya kazi.
KUSUDI LA KUANDIKA BARUA YA KIKAZI
Wakati
unaandika barua, unatakiwa:
- kujitambulisha
- Orodhesha kazi unayotaka kuomba
- Onyesha ujuzi na uzoefu wako
kuwa vinaendana na kazi unayoomba.
- Mshawishi msomaji aendelee
kusoma na CV yako
Barua ya kikazi inatakiwa iwe na urefu gani?
Ifanye
iwe fupi. Barua ni ufupisho wa CV yako kwaiyo usiandike zaidi ya ukurasa mmoja.
Linganisha barua yako iendane na kazi
unayoomba.
Tumia
barua tofauti kwa kila kazi unayoomba, barua yako inatakiwa ionyeshe unaijua
kazi unayoiomba. Na kipi mwajiri anataka kukiona
Kwa
kufanya hivi, Onyesha ujuzi na ubora wako ambao unaendana na mahitaji ya kazi
unayoomba.
1. Tafuta mtu sahihi ambaye anapaswa
kuandikiwa barua.
Mara
nyingi kwenye matangazo ya kazi huwa wanaandika mtu anayepaswa kuandikiwa
barua. Likini kuna baadhi ya barua ambazo unatakiwa uwandike bila ya kuona
Tangazo unapaswa utafute mtu sahihi ambaye atasoma na kuifanyia kazi barua
yako.
2. Tafuta zaidi maelezo ya kutosha kuhusiana na
kazi hiyo
3. Tafuta maelezo zaidi ya kuhusu Kampuni
unayoomba kazi
- Kama unajua jina la kampuni
unayoomba kazi tafuta maelezo yake mtandaoni au jaribu kuuliza watu
- Kama kampuni ina tovuti ingia
na uangalie sehemu ya About/Kuhusu na usome kwa makini kampuni au taasisi
inajishughulisha na nini.
Kipi kinatakiwa kuwepo kwenye barua yako
Hivi
ni vitu vinavyotakiwa kwenye barua yako ya kikazi
Jina lako, Anuani yako na mawasiliano yako.
Andika
jina, anuani na mawasiliano yako juu kabisa ya barua yako. Haitoshi tu kuweka
anuani yako pekee ila weka na email na namba za simu.
Anuani ya kampuni au jina la mtu inayemfikia
Hakikisha
unaandika anuani sahihi kwa mtu sahihi.
Jina la kazi unayoomba.
Mwanzo
wa barua unatakiwa uandike kazi unayoomba hasa kwenye kichwa cha barua.
Pia
unaweza ukaandika mwanzo wa aya ya kwanza.
Orodhesha ujuzi wako unafanana na Ajira au
kazi unayoomba.
Eleza
kwa ufupi kuhusu ujuzi wako unaoendana na kazi unayoomba.
Kumbuka
kuwa kama unasema una ujuzi unatakiwa useme jinsi utakavoutumia iwapo utapata
kazi hiyo na kama ulishawahi kuutumia huo ujuzi.
Andika kwanini wewe unafaa zaidi kwa kazi hiyo.
Baada
ya kuorothesha ujuzi wako unatakiwa uelezee kwanini wewe unafaa zaidi kwa kazi
hiyo, kipi kitu cha pekee ambacho unacho kitakachowavutia waajiri wako ili
wakuajiri.
Waombe
waajiri wako wakutafute
Barua
yako lazima imalize kwa kuomba waajiri wako wasome CV yako pia waombe wafanye
mawasiliano na wewe.
Mfano
nimeambatanisha na CV yangu, ni mategemeo yangu nitasikia chochote kutoka kwenu.
Kipi kinatakiwa kisiwepo kwenye barua yako ya
kikazi.
Kuna
vitu ambavyo havitakiwi kuwepo katika barua yako ya kikazi.
Kukosea baadhi ya maneno
Makosa
ya kimaandishi kwenye barua yako kama kukosea baadhi ya maneno au kuunganisha
maneno.
Hakiki
barua yako zaidi ya mara mbili kabla haujaituma kama umeandika jina la kampuni
hakikisha umeandika kwa usahihi, kama sehemu au eneo hakikisha umeandika kwa
usahihi.
Kuambatanisha CV yako yote kwenye barua
Usi
kopi na kuweka CV yako yote kwenye barua yako ya kikazi. Kumbuka barua yako ni
ufupisho wa kile kilichopo kwenye CV.
Matumizi ya mimi yaliyozidi
Jaribu
kutokutumia maneno kama mimi ninaamini, mimi nina, mimi nip, hapa siyo. Kumbuka
hapa siyo kuhusu wewe ila ni kujielezea ni jinsi gani unaweza kumsaidia muajiri
ili atimize malengo yake iwapo atakuchagua wewe kuwa mfanyakazi wake.
Baada
ya kuandika barua yako jitahidi kuipitia tena na jaribu kuondoa sentensi zote
zilizojaa neon la mimi.
Epuka kutaja maombi yako ya kazi nyingine.
Kiukweli
huwa tunaomba kazi zaidi ya moja ni vizuri kutokueleza kuwa umeomba na kazi
nyingine kwa watu wengine inayoendana na hiyo, lengo letu ni kumshawishi
muajiri kuwa una uchu na ukwasi wa kazi hiyo.
Aina tofauti ya Barua za kikazi
- Barua ya kikazi ambayo hauna
ujuzi wowote (fresh from school)
- Barua ya kikazi ambayo tayari
una ujuzi (ulishafanya kazi sehemu)
- Barua ya kikazi ambayo CV
haihitajiki
- Barua ya kikazi
ambayo haina Tangazo.
KWA MAHITAJI YA BARUA ZA KIKAZI
MUONGOZO/SAMPLE 300/=
KUANDIKIWA BARUA NZIMA 500/=
Comments
Post a Comment